Siku ya Nane
*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona ukiwa umesujud mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana, ninapotafakari paji la uso wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka katika taji la miiba la Yesu Kristo, mchumba wako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe kweli ni mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa. Hivyo sikukosea nilipoweka imani yangu yote kwako, na nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoombakutoka kwako. Naamini sala hii kwako wewe mama mpenzi sana haitapotea bure. Wewe uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo **(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).**
Mungu hakukatalii wewe kitu chochote; kwa maombezi yako, miujiza hufanywa, neema na fadhila maalumu hupatikana. Hivyo, kwa moyo wangu wote na matumaini ya dhati, ninasubiri nikitegemea kupata haya niliyoomba kwa Bwana Mungu.
*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*
*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130
Day Eight
*In the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.*
O holy image of the glorious Cross, when I behold you kneeling before the sacred feet of the Lord, when I contemplate your forehead wounded by a thorn taken from the crown of thorns of Jesus Christ, your beloved Spouse, my faith in you blossoms in a wondrous way. Truly, you are the chosen servant of God. God has bestowed upon you the mark of His kingdom; He has sanctified you and made you wholly His own. Therefore, I was not mistaken when I placed all my trust in you, and when I placed myself completely under your most merciful protection. And now is the favourable time for you to help me, knowing the needs and helps which I ask from you. I believe that this prayer to you, most beloved mother, will not be in vain. You, wonder-worker, benefactress of heavenly things, hope of all humanity: I pray and beseech you, by the merits of your love for Jesus Christ our Saviour, intercede for me, that I may be granted these things which I ask: **(here make the need you desire to ask of God through Saint Rita).**
God refuses you nothing; through your intercession, miracles are performed, and special graces and favours are obtained. Therefore, with all my heart and with sincere hope, I wait, trusting that I shall receive from the Lord God these things for which I have prayed.
*Our Father (3), Hail Mary (3), Glory Be (3)*
Through Saint Rita: may fevers, sores and plague, the germs of many diseases, demons, and wrath disappear. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Through your intercession: thunder, earthquakes, and fire have no power. By your holiness, every snare, every great danger, and every threat disappears. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Spain proclaims you the Saint of impossible cases. Many people sing your praises. Cascia glorifies your name. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
To God the Holy One, and to His Son, be praise, glory, and honour; praise throughout all ages of everlasting love. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
*V: You have marked, O Lord, Your servant Rita.*
*R: With the seal of love and suffering.*
*LET US PRAY:* O God, who graciously adorned Saint Rita with grace, so that she loved her enemies and bore in her soul and upon her forehead the marks of love and suffering: we ask You, through her intercession, for the grace to forgive our enemies and to meditate upon the sorrows of Your Passion, so that we may receive the reward You have promised to the meek and to those who suffer. You who live and reign, forever and ever. Amen.
After completing this section, pray the Litany of St. Rita, the Litany of the Thorn of St. Rita, Psalm 51, or Psalm 130.