Siku ya Saba

*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*

Ee mpendwa Rita, ambaye maisha yako yalikuwa ya huzuni. Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu makali. Naomba sala zangu, uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo wako mpole ili uweze kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote uliionesha kwa jirani, maneno ya amani na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa watu wote vinivute kukuelekea wewe uliye katika mbingu unakoishi na kuwa mwombezi wa watu wote waliokata tamaa. Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo kinarudi nyuma, vipofu wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza wanaponyeshwa na ulemavu wote wa roho na mwili unaondoka kabisa. Je! nipo peke yangu nisiyefarijiwa kwa maombezi yako? Sitaamini wala siwezi kuamini hivyo. Nami naamini kwa dhati usimamizi wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Nina matumaini makubwa kuwa nitapata amani, moyo wangu utatulia, na fadhila ninazoomba nitajaliwa **(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).**

*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*

Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*

*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.

Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130