Siku ya Sita
*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Nafahamu kuwa sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa na wingu zisiweze kufika katika kiti chako cha enzi. Dhambi zangu ni sababu ya adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri wa kuelekeza sauti yangu kwa Yesu. Kwa kuwa mara nyingi sikuthamini huruma yake. Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki. Mkono wake wa haki umenielekea. Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha wake kwani nimegubikwa na huzuni kubwa. Pasipo matumaini ninayalilia madhambi yangu. Niambie Mtakatifu Rita; Je, niendelee kukata tamaa? Hapana. Bwana wetu Yesu Kristo amekuteua kuwa mtetezi wake mwenye nguvu, ili uniombee kwa Yesu wangu aliye juu, msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia safi ya kutomtendea dhambi tena. Kwa uamuzi huu thabiti, wa midomo yangu na moyo wangu, nakuelekea wewe. Ee Mtakatifu mtenda miujiza, uniombee kwa Bwana Yesu, fadhila ambazo nazihitaji sana **(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).**
Katika muda huu wa uchovu mkubwa, huzuni na kuachwa pweke; Ee Rita, neno lako kwa Yesu litafungua huruma na msamaha wake. Sema neno na Yesu atakusikia.
*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*
*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130
Day Six
*In the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.*
I know that because of my sins, my prayers have been covered by a cloud and cannot reach your throne. My sins are the cause of my great punishments. I do not have the courage to raise my voice to Jesus, because many times I failed to value His mercy. And now I see His great and just power. His righteous hand is turned toward me. I recognize that I do not deserve the blessings of His forgiveness, for I am overwhelmed by great sorrow. Without hope, I weep over my sins. Tell me, Saint Rita: shall I continue to despair? No. Our Lord Jesus Christ has chosen you as His powerful advocate, so that you may intercede for me before my Jesus on high, obtaining forgiveness for my grave faults and a pure intention never to offend Him again. With this firm resolve of my lips and my heart, I turn to you. O wonder-working Saint, intercede for me before the Lord Jesus for the virtues and graces which I so greatly need: **(here make the need you desire to ask of God through Saint Rita).**
In this time of great weariness, sorrow, and loneliness, O Rita, your word to Jesus will open His mercy and forgiveness. Speak one word, and Jesus will hear you.
*Our Father (3), Hail Mary (3), Glory Be (3)*
Through Saint Rita: may fevers, sores and plague, the germs of many diseases, demons, and wrath disappear. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Through your intercession: thunder, earthquakes, and fire have no power. By your holiness, every snare, every great danger, and every threat disappears. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Spain proclaims you the Saint of impossible cases. Many people sing your praises. Cascia glorifies your name. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
To God the Holy One, and to His Son, be praise, glory, and honour; praise throughout all ages of everlasting love. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
*V: You have marked, O Lord, Your servant Rita.*
*R: With the seal of love and suffering.*
*LET US PRAY:* O God, who graciously adorned Saint Rita with grace, so that she loved her enemies and bore in her soul and upon her forehead the marks of love and suffering: we ask You, through her intercession, for the grace to forgive our enemies and to meditate upon the sorrows of Your Passion, so that we may receive the reward You have promised to the meek and to those who suffer. You who live and reign, forever and ever. Amen.
After completing this section, pray the Litany of St. Rita, the Litany of the Thorn of St. Rita, Psalm 51, or Psalm 130.