Siku ya Nne
*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Ee Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana, na wakili wa waliokata tamaa. Hizi ni sifa safi zenye kujaa tumaini kwa roho zenyekujaribiwa na uchungu. Kwako wewe Mtakatifu Rita wa Kashia, ambaye wakati tunapojikuta pweke katika maisha yetu, tunapozungukwa na huzuni na kifo, wewe watujia kama mtunza bustani kutoka mbinguni kutuletea ndani ya mioyo yetu iliyokauka tumaini na maji yaliyo hai. Ee tumaini la moyo wangu ulikauka kutokana na msongo mkubwa wa huzuni. Uzito wa maafa umenielemea, mashaka yananiogofya na sijui nielekee wapi kutafuta msaada ninaohitaji. Kwako wewe Rita mwema ninakuamini sana na kukutegemea, nakuja nikiwa na uhakika utanisikiliza. Kwa nguvu ya maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, natumaini kusikilizwa katika ombi langu **(hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).**
Jioneshe tena kuwa u mwenye nguvu na huruma. Nithibitishie pia kuwa ni kweli kama wafuasi wako wanavyokukiri kuwa Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana na wakili wa waliokata tamaa.
*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*
*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130
Day Four
*In the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.*
O Saint of impossible cases, and advocate of those who have lost hope: these are pure titles, full of hope for souls tried by sorrow. To you, Saint Rita of Cascia, who, when we find ourselves alone in our lives, surrounded by sorrow and death, come to us like a gardener from heaven, bringing into our dry hearts hope and living water. O hope of my heart, which has dried up because of the heavy burden of sorrow: the weight of misfortune has overwhelmed me, doubts frighten me, and I do not know where to turn to seek the help I need. To you, good Rita, in whom I greatly trust and on whom I rely, I come with confidence that you will hear me. Through the power of your intercession before the throne of God, I hope to be heard in my petition: **(here make the need you desire to ask of God through Saint Rita).**
Show yourself once more to be powerful and merciful. Prove to me also that it is true, as your followers confess, that you are the Saint of impossible cases and the advocate of those who have lost hope.
*Our Father (3), Hail Mary (3), Glory Be (3)*
Through Saint Rita: may fevers, sores and plague, the germs of many diseases, demons, and wrath disappear. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Through your intercession: thunder, earthquakes, and fire have no power. By your holiness, every snare, every great danger, and every threat disappears. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Spain proclaims you the Saint of impossible cases. Many people sing your praises. Cascia glorifies your name. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
To God the Holy One, and to His Son, be praise, glory, and honour; praise throughout all ages of everlasting love. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
*V: You have marked, O Lord, Your servant Rita.*
*R: With the seal of love and suffering.*
*LET US PRAY:* O God, who graciously adorned Saint Rita with grace, so that she loved her enemies and bore in her soul and upon her forehead the marks of love and suffering: we ask You, through her intercession, for the grace to forgive our enemies and to meditate upon the sorrows of Your Passion, so that we may receive the reward You have promised to the meek and to those who suffer. You who live and reign, forever and ever. Amen.
After completing this section, pray the Litany of St. Rita, the Litany of the Thorn of St. Rita, Psalm 51, or Psalm 130.