Siku ya Tatu
*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa pumziko, huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu, najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Rita, unayeng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usiokifani katika nguvu na nguzo za Kanisa Katoliki, natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini, kwa hamu nangojea, kupata kile nikiombacho (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Nifikishie ombi langu kwa Yesu wa msalaba. Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopitia majaribu, kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa, uliyomtolea Mungu wana wako, ukiomba wasinajisiwe kwa dhambi. Uniombee kwa Mungu. Hicho ni kifo dini cha moyo wako. Kwa njia ya mateso uliyochagua yaani kukaa ndani utawani maisha yako; kupitia mateso ambayo Bwana Yesu Kristo aliruhusu yakupate ili utakaswe katika majonzi yako; kwa njia ya majaribu mengi yaliyokupata na sadaka nyingi ulizotoa; uniombee ili nijaliwe kupewa ombi langu ninalongojea kwa hamu.
*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*
*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130
Day Three
*In the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.*
I look here and there without finding any place of rest, while my eyes are overshadowed by sorrow. No hope of this world brings joy to my heart, which is weighed down with grief; I feel utterly lost. But you, beloved Saint Rita, who shine like a star giving incomparable light among the powers and pillars of the Catholic Church, I know that you illumine my dark path and give courage to my heart that mourns in sorrow. I believe in you, and with longing I await the granting of what I ask: **(here make the need you desire to ask of God through Saint Rita).**
Present my petition to Jesus of the Cross. I remember that difficult time for you, when your heart passed through trials, when in obedience you accepted marriage to a man who tormented you and even threatened your life. Yet you loved him greatly, and when he died you mourned his death with deep sorrow. By the heroic sacrifice which you offered to God in your sons, praying that they might not be defiled by sin, intercede for me before God. This is the martyrdom of your heart. Through the suffering you chose, namely to live your life within the convent; through the sufferings which the Lord Jesus Christ permitted to come upon you so that you might be purified in your sorrows; through the many trials that befell you and the many sacrifices you offered: intercede for me, that I may be granted the petition for which I wait with longing.
*Our Father (3), Hail Mary (3), Glory Be (3)*
Through Saint Rita: may fevers, sores and plague, the germs of many diseases, demons, and wrath disappear. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Through your intercession: thunder, earthquakes, and fire have no power. By your holiness, every snare, every great danger, and every threat disappears. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Spain proclaims you the Saint of impossible cases. Many people sing your praises. Cascia glorifies your name. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
To God the Holy One, and to His Son, be praise, glory, and honour; praise throughout all ages of everlasting love. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
*V: You have marked, O Lord, Your servant Rita.*
*R: With the seal of love and suffering.*
*LET US PRAY:* O God, who graciously adorned Saint Rita with grace, so that she loved her enemies and bore in her soul and upon her forehead the marks of love and suffering: we ask You, through her intercession, for the grace to forgive our enemies and to meditate upon the sorrows of Your Passion, so that we may receive the reward You have promised to the meek and to those who suffer. You who live and reign, forever and ever. Amen.
After completing this section, pray the Litany of St. Rita, the Litany of the Thorn of St. Rita, Psalm 51, or Psalm 130.