Siku ya Kumi na Moja

*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*

Ee Moyo mpendevu wa Yesu, ulio daima na utajiri na ukarimu wa huruma isiyo na mwisho. Na ambaye ulimwambia nabii kuwa sikifurahi kifo cha mtu mwovu bali ageuke na kuishi, uniangalie katika unyonge wangu. Nakushukuru wewe kwa moyo wangu wote kwa neema za pekee ulionijalia kupitia fadhila za mtumishi wako mteule, Mtakatifu Rita wa Kashia. Je? Nitakurudishia nini, Ee Bwana, kwa upendo ulionijalia? Ee Mungu wangu, sitaacha daima kukushukuru, Wewe ambaye daima umekuwa mwema kwa wote wanaokudharau.

Nawe mpenzi Mtakatifu Rita, nikulipeje fadhila ulizonijalia? Moyo wangu umejaa furaha isiyo na kifani. Nitakushukuru bila mwisho. Ee Mtakatifu mwema, uliye karibu na Bwana wetu; nipelekee shukrani zangu kwa Yesu mpenzi. Mwambie kuwa moyoni mwangu zimejaa shukruani zangu kwake na kwako na kuwa daima nitaichukia dhambi, ili niendelee kufaidi huruma yake na maongozi yake ya mbinguni.

*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*

Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishiwako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*

*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapatarohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.

Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mt. Rita