Siku ya Kumi

*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*

Baba wa milele! Ambaye huruma yako haina mwisho, na wema wako ni wa milele. Niangalie nikikusujudia kwa unyenyekevu mbele ya kiti chako cha enzi kitukufu. Nainua kutoka chini ya moyo wangu utenzi wakukushukuru kwa upendo ulionijalia kupitia mtumishi wako Mtakatifu Rita wa Kashia. Natambua, Ee Mungu wangu kuwa sistahili kupata fadhila ulizonikirimia na kwa kutokujali mapungufu yangu bali umesikiliza sala yangu kwa maombezi ya Mtakatifu Rita wa Kashia.

Ee Mtakatifu Rita, mfanya miujiza maarufu wa Kanisa Katoliki. Kwako ninakutolea shukrani zangu za dhati. Kinywa changu hakina maneno ya kutosha ya kueleza jinsininavyojisikia moyoni mwangu. Ee Mtakatifu mpenzi; ni kweli kwamba wote wanaotumainia maombezi yako hawakatishwi tamaa. Nijaze daima neema ambayo naweza kupata kupitia huruma ya Mungu na unijalie ulinzi wako katika maisha na kifo.

*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*

Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*

*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishiwako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*

*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapatarohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.

Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mt. Rita