Siku ya 6
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
"Leo uniletee ROHO ZA WAPOLE NA WANYENYEKEVU NA ROHO ZA WATOTO WADOGO, na uwazamishie katika huruma yangu. Roho hizi zinafanana kwa karibu sana na Moyo wangu. Zilinitia nguvu wakati wa uchungu wangu mkali. Niliwaona kama Malaika wa duniani, watakaokesha katika madhabahu zangu. Ninamimina juu yao mafuriko yote ya neema. Ni roho mnyenyekevu tu aliye na uwezo wa kuipokea neema yangu. Naziamini roho nyenyekevu kwa namna ya pekee."
Yesu Mwenye Huruma Sana, wewe mwenyewe umesema, "Jifunzeni kwangu kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo." Zipokee katika makao ya Moyo wako wenye Huruma Sana roho zote za wapole na wanyenyekevu na roho za watoto wadogo. Roho hizi hufanya mbingu yote ishikwe na furaha kuu, nazo ni vipenzi vya Baba wa mbinguni. Ni shada lenye harufu nzuri mbele ya kiti cha enzi cha Mungu; Mungu mwenyewe hupendezwa na harufu yake. Roho hizi zina makao ya kudumu katika Moyo wako wenye Huruma Sana, ee Yesu, nazo huimba bila kukoma wimbo wa upendo na huruma.
Baba wa Milele, elekeza macho yako ya huruma juu ya roho za wapole, juu ya roho za wanyenyekevu, na juu ya watoto wadogo waliofunikwa katika makao ambayo ni Moyo wa Yesu wenye Huruma Sana. Roho hizi zinafanana kwa karibu kabisa na Mwanao. Harufu yao hupanda kutoka duniani na kufika kwenye kiti chako cha enzi. Baba wa huruma na wa wema wote, ninakuomba kwa upendo ulio nao kwa roho hizi na kwa furaha unayopata ndani yao: Ubariki ulimwengu wote, ili roho zote kwa pamoja ziimbe sifa za huruma yako kwa nyakati zisizo na mwisho.
Amina.
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
Day 6
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.
"Today bring to Me THE MEEK AND HUMBLE SOULS AND THE SOULS OF LITTLE CHILDREN, and immerse them in My mercy. These souls most closely resemble My Heart. They strengthened Me during My bitter agony. I saw them as earthly Angels, who will keep vigil at My altars. I pour out upon them whole torrents of grace. Only the humble soul is capable of receiving My grace. I favor humble souls with My confidence."
Most Merciful Jesus, You yourself have said, "Learn from Me for I am meek and humble of heart." Receive into the abode of Your Most Compassionate Heart all meek and humble souls and the souls of little children. These souls send all heaven into ecstasy and they are the heavenly Father's favorites. They are a sweet-smelling bouquet before the throne of God; God Himself takes delight in their fragrance. These souls have a permanent abode in Your Most Compassionate Heart, O Jesus, and they unceasingly sing out a hymn of love and mercy.
Eternal Father, turn Your merciful gaze upon meek souls, upon humble souls, and upon little children who are enfolded in the abode which is the Most Compassionate Heart of Jesus. These souls bear the closest resemblance to Your Son. Their fragrance rises from the earth and reaches Your very throne. Father of mercy and of all goodness, I beg You by the love You bear these souls and by the delight You take in them: Bless the whole world, that all souls together may sing out the praises of Your mercy for endless ages.
Amen.
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.