Siku ya 4

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

"Leo uniletee WALE WASIOMWAMINI MUNGU NA WALE AMBAO BADO HAWANIJUI. Niliwafikiria pia wakati wa Mateso yangu makali, na bidii yao ya baadaye iliufariji Moyo wangu. Wazamishie katika bahari ya huruma yangu."

Yesu Mwenye Huruma Sana, wewe ni Mwanga wa ulimwengu wote. Zipokee katika makao ya Moyo wako wenye Huruma Sana roho za wale wasiomuamini Mungu na za wale ambao bado hawakujui. Miale ya neema yako iwaangazie ili wao pia, pamoja nasi, waweze kuitukuza huruma yako ya ajabu; wala usiwaache watoke katika makao ambayo ni Moyo wako wenye Huruma Sana.

Baba wa Milele, elekeza macho yako ya huruma juu ya roho za wale wasiokuamini, na za wale ambao bado hawakujui, lakini ambao wamefungiwa ndani ya Moyo wa Yesu wenye Huruma Sana. Wavutie kwenye mwanga wa Injili. Roho hizi hazijui furaha kuu iliyopo katika kukupenda. Ujalia kwamba wao pia waweze kuitukuza ukarimu wa huruma yako kwa nyakati zisizo na mwisho.

Amina.

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.