Siku ya 3
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
"Leo uniletee ROHO ZOTE ZA WAUMINI WACHAMUNGU NA WAAMINIFU, na uwazamishie katika bahari ya huruma yangu. Roho hizi ziliniletea faraja katika Njia ya Msalaba. Zilikuwa tone la faraja katikati ya bahari ya uchungu."
Yesu Mwenye Huruma Sana, kutoka hazina ya huruma yako, unatoa neema zako kwa wingi mkubwa kwa kila mmoja na kwa wote. Utupokee katika makao ya Moyo wako wenye Huruma Sana wala usituache kamwe tutoke humo. Tunakuomba neema hii kwa ule upendo wa ajabu kabisa kwa Baba wa mbinguni ambao Moyo wako huwaka nao kwa nguvu sana.
Baba wa Milele, elekeza macho yako ya huruma juu ya roho za waaminifu, kama juu ya urithi wa Mwanao. Kwa ajili ya Mateso yake yenye uchungu, uwajalie baraka yako na uwazungushie ulinzi wako wa daima. Hivyo wasianguke kamwe katika upendo wala kupoteza hazina ya imani takatifu; bali, pamoja na majeshi yote ya Malaika na Watakatifu, waitukuze huruma yako isiyo na mipaka kwa nyakati zisizo na mwisho.
Amina.
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
Day 3
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.
"Today bring to Me ALL DEVOUT AND FAITHFUL SOULS, and immerse them in the ocean of My mercy. The souls brought Me consolation on the Way of the Cross. They were that drop of consolation in the midst of an ocean of bitterness."
Most Merciful Jesus, from the treasury of Your mercy, You impart Your graces in great abundance to each and all. Receive us into the abode of Your Most Compassionate Heart and never let us escape from It. We beg this grace of You by that most wondrous love for the heavenly Father with which Your Heart burns so fiercely.
Eternal Father, turn Your merciful gaze upon faithful souls, as upon the inheritance of Your Son. For the sake of His sorrowful Passion, grant them Your blessing and surround them with Your constant protection. Thus may they never fail in love or lose the treasure of the holy faith, but rather, with all the hosts of Angels and Saints, may they glorify Your boundless mercy for endless ages.
Amen.
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.