Siku ya Pili
*Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.*
Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita wa Kashia. Naona njia ya maisha yako imejaa majaribu na miiba mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua moyo wako vipande vipande. Ee Rita uliye kweli shahidi wa maumivu makali. Uliyeonja tone kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu makali. Nafikiria juu ya moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa maombezi yako (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Wewe unajua maana ya moyo unaovuja damu. Unajua pia kifodini cha roho. Umeumizwa sana na kuteseka sana. Kwa njia ya mateso hayo nakuomba unisaidie katika mahangaiko yangu. Je si kweli kwamba wakati huu mgumu, Bwana wetu Yesu ametuandalia njia ya kujipatia neema; kupitia miujiza ambayo binadamu wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi yako wakafanikiwa?
Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie roho iliyo pondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako. Ninakutumainia, Ee Mtakatifu Rita. Niombee kwa Yesu mbinguni ili nipate kupokea yote ninayomwomba Mungu kwa maombezi yako yenye nguvu.
*Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)*
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadabu vitoweke. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na vivete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi, na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na vivete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na vivete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. *Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na vivete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.*
*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*
*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo uliotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130
Day Two
*In the Name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.*
O wonder-working Saint Rita of Cascia, I see that the path of your life was filled with many trials and piercing thorns, which I fear tore your heart into pieces. O Rita, true martyr of bitter sorrow, you who tasted, drop by drop, until you had drained the whole chalice of deep suffering: I think upon your heart, utterly worn out. I turn to you and ask God through your intercession: (here make the need you desire to ask of God through Saint Rita).
You know the meaning of a bleeding heart. You also know the martyrdom of the soul. You were wounded greatly and suffered deeply. Through those sufferings, I beg you to help me in my anxieties. Is it not true that in this difficult time our Lord Jesus has prepared for us a way of obtaining grace, through the miracles which human beings may ask of you with hope and, through your intercession, may obtain?
O beloved Saint, look upon this crushed soul, weeping and sorrowing before you. I place my trust in you, O Saint Rita. Intercede for me before Jesus in heaven, that I may receive all that I ask of God through your powerful intercession.
*Our Father (3), Hail Mary (3), Glory Be (3)*
Through Saint Rita: may fevers, sores and plague, the germs of many diseases, demons, and wrath disappear. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Through your intercession: thunder, earthquakes, and fire have no power. By your holiness, every snare, every great danger, and every threat disappears. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
Spain proclaims you the Saint of impossible cases. Many people sing your praises. Cascia glorifies your name. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
To God the Holy One, and to His Son, be praise, glory, and honour; praise throughout all ages of everlasting love. *You help the blind, the deaf, the mute, and the lame; children earnestly implore you, and the dead are restored to life.*
*V: You have marked, O Lord, Your servant Rita.*
*R: With the seal of love and suffering.*
*LET US PRAY:* O God, who graciously adorned Saint Rita with grace, so that she loved her enemies and bore in her soul and upon her forehead the marks of love and suffering: we ask You, through her intercession, for the grace to forgive our enemies and to meditate upon the sorrows of Your Passion, so that we may receive the reward You have promised to the meek and to those who suffer. You who live and reign, forever and ever. Amen.
After completing this section, pray the Litany of St. Rita, the Litany of the Thorn of St. Rita, Psalm 51, or Psalm 130.