Siku ya Kwanza

Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Ee Mtakatifu Rita mfanya miujiza, uniangalie kwa macho yako yenye huruma, mimi ninaye teseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu umezungukwa na miiba. Yaone macho yangu, Ee Mtakatifu Rita, kuwa hayatoki machozi tena, kwani machozi mengi yamenitoka!
Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu? Ujue! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na dhihirisha ukuu wa waliokata tamaa? Basi toka kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba hihaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Kila mtu anasifiwa utakatifu wako. Kila mtu anasimilia maajubu na miujiza yako. Kila mtu anayotenda kwa njia yako. Je, mimi tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uniombee kwa Bwana Yesu ili anionee huruma na kunisaidia katika masumbuko na mahangaiko yangu. Kwa maombezi yako, Ee Mtakatifu Rita, niweze kupokea kile moyo wangu unatamani sana.

Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)

Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na fauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia viwete; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai

Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mtego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa Mungu Mtakatifu, na Kwa Mwanae ziwe sifa, Utukufu na heshima, Sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

*K: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.*
*W: Kwa mhuri wa upendo na mateso.*

*TUOMBE:* Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo uliotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.

Baada ya kumaliza sehemu hii, sali Litania ya Mt. Rita, Litania ya Mwiba wa Mt. Rita, Zaburi ya 51 au Zaburi 130