Siku ya 8
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
"Leo uniletee ROHO ZINAZOZUILIWA TOHARANI, na uwazamishie katika kina cha huruma yangu. Mifuriko ya Damu yangu ipoze miali yao inayowaka. Roho hizi zote zinapendwa sana nami. Zinalipa fidia kwa haki yangu. Iko katika uwezo wako kuziletea nafuu. Chota rehema zote kutoka hazina ya Kanisa langu na uzitoe kwa ajili yao. Laiti ungejua mateso wanayoyapata, ungeendelea kuwatoea sadaka za roho na kulipa deni lao kwa haki yangu."
Yesu Mwenye Huruma Sana, wewe mwenyewe umesema kwamba unatamani huruma; kwa hiyo ninazileta katika makao ya Moyo wako wenye Huruma Sana roho zilizo Toharani, roho zilizo karibu sana nawe, lakini ambazo bado zinapaswa kulipa fidia kwa haki yako. Mito ya Damu na Maji iliyobubujika kutoka Moyoni mwako izime miali ya Toharani, ili huko pia uwezo wa huruma yako uweze kusherehekewa.
Baba wa Milele, elekeza macho yako ya huruma juu ya roho zinazoteseka Toharani, ambazo zimefunikwa katika Moyo wa Yesu wenye Huruma Sana. Ninakuomba, kwa Mateso yenye uchungu ya Yesu Mwanao, na kwa uchungu wote ambao Nafsi yake takatifu kabisa ilifurika nao: Udhihirishe huruma yako kwa roho zilizo chini ya uchunguzi wako wa haki. Usiziangalie kwa njia nyingine yoyote ila tu kupitia Majeraha ya Yesu, Mwanao mpendwa sana; kwa maana tunaamini kwa uthabiti kwamba hakuna kikomo kwa wema na huruma yako.
Amina.
Sali Chapleti ya Huruma ya Mungu.
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.
Day 8
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.
"Today bring to Me THE SOULS WHO ARE DETAINED IN PURGATORY, and immerse them in the abyss of My mercy. Let the torrents of My Blood cool down their scorching flames. All these souls are greatly loved by Me. They are making retribution to My justice. It is in your power to bring them relief. Draw all the indulgences from the treasury of My Church and offer them on their behalf. Oh, if you only knew the torments they suffer, you would continually offer for them the alms of the spirit and pay off their debt to My justice."
Most Merciful Jesus, You Yourself have said that You desire mercy; so I bring into the abode of Your Most Compassionate Heart the souls in Purgatory, souls who are very dear to You, and yet, who must make retribution to Your justice. May the streams of Blood and Water which gushed forth from Your Heart put out the flames of Purgatory, that there, too, the power of Your mercy may be celebrated.
Eternal Father, turn Your merciful gaze upon the souls suffering in Purgatory, who are enfolded in the Most Compassionate Heart of Jesus. I beg You, by the sorrowful Passion of Jesus Your Son, and by all the bitterness with which His most sacred Soul was flooded: Manifest Your mercy to the souls who are under Your just scrutiny. Look upon them in no other way but only through the Wounds of Jesus, Your dearly beloved Son; for we firmly believe that there is no limit to Your goodness and compassion.
Amen.
Pray the Divine Mercy Chaplet.
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit. Amen.