Siku ya 1

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

"Leo uniletee WANADAMU WOTE, HASA WAKOSEFU WOTE, na uwazamishie katika bahari ya huruma yangu. Kwa njia hii utanifariji katika huzuni kali ambayo upotevu wa roho hunizamisha ndani yake."

Yesu Mwenye Huruma Sana, ambaye asili yako yenyewe ni kutuhurumia na kutusamehe, usitazame dhambi zetu bali utazame tumaini letu tunaloliweka katika wema wako usio na mwisho. Utupokee sisi sote katika makao ya Moyo wako wenye Huruma Sana, wala usituache kamwe tutoke humo. Tunakuomba hili kwa upendo wako unaokuunganisha na Baba na Roho Mtakatifu.

Baba wa Milele, elekeza macho yako ya huruma juu ya wanadamu wote, hasa juu ya wakosefu maskini, wote wakiwa wamefunikwa ndani ya Moyo wa Yesu wenye Huruma Sana. Kwa ajili ya Mateso yake yenye uchungu, utuonyeshe huruma yako, ili tuweze kusifu uweza mkuu wa huruma yako milele na milele.

Amina.

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.