Matendo ya Mwanga

Alhamisi

  1. Tendo la kwanza: Yesu anabatizwa Mto Jordani.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
  2. Tendo la pili: Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
  3. Tendo la tatu: Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
  4. Tendo la nne: Yesu anageuka sura.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung'arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
  5. Tendo la tano: Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
← Back to mysteries of the Rosary