Matendo ya Furaha

Jumatatu, Jumamosi

  1. Tendo la kwanza: Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
  2. Tendo la pili: Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
  3. Tendo la tatu: Yesu anazaliwa Betlehemu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.
  4. Tendo la nne: Yesu anatolewa hekaluni.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
  5. Tendo la tano: Maria anamkuta Yesu hekaluni.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
← Back to mysteries of the Rosary