Siku ya 3

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Amina.

Enyi Mitume watakatifu, ninyi mlioitwa kwanza na Yesu kuwa wafuasi wake, mnaonyesha maana ya kuwa mfuasi wa kweli wa Kristo. Niombeeni ili niwe tayari zaidi kumpokea Roho mliyempokea siku ya Pentekoste, nipate kuwa na bidii ya kukua kama mfuasi wa Kristo. Ninaomba mziweke haja zangu mbele ya Mungu.

(Taja nia zako hapa)

Mtakatifu Petro, utuombee.

Mtakatifu Andrea, utuombee.

Mtakatifu Yakobo, utuombee.

Mtakatifu Yohane, utuombee.

Mtakatifu Filipo, utuombee.

Mtakatifu Yuda Thadei, utuombee.

Mtakatifu Bartolomayo, utuombee.

Mtakatifu Tomaso, utuombee.

Mtakatifu Yakobo, utuombee.

Mtakatifu Mathayo, utuombee.

Mtakatifu Simoni, utuombee.

Mtakatifu Mathia, utuombee.

Amina.

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Amina.