Siku ya 4: Subira
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
Amina.
Subira
Tuiname kwa unyenyekevu mbele ya nguvu na ukuu wa Roho Mtakatifu. Tuabudu Utatu Mtakatifu na leo tumtukuze Mfariji, Mtetezi wetu.
Ee Roho Mtakatifu, kwa uwezo wako Kristo alifufuliwa kutoka wafu ili kutuokoa sisi sote. Kwa neema yako, miujiza hutendeka kwa jina la Yesu. Kwa upendo wako, tunalindwa na uovu. Kwa hiyo, tunaomba kwa unyenyekevu na kwa moyo wa mwombaji maskini zawadi yako ya Subira ndani yetu.
Ee Roho Mtakatifu, unawapa kwa ukarimu wale wanaokuomba. Tafadhali utujalie subira ya Watakatifu walioko pamoja nawe mbinguni. Utusaidie kuvumilia yote kwa subira ya milele inayowezekana tu kwa msaada wako.
Roho Mtakatifu, tunakuomba neema ya [Taja nia yako hapa].
Amina.
Uje Roho Mtakatifu, ujaze mioyo ya waamini wako na uwashe ndani yao moto wa upendo wako. Utume Roho wako, nao wataumbwa. Nawe utaufanya upya uso wa dunia.
Ee Mungu, uliyezifundisha nyoyo za waamini kwa mwanga wa Roho Mtakatifu, utujalie kwa Roho huyo huyo tuwe wenye hekima ya kweli na tufurahie daima faraja zake, kwa njia ya Kristo Bwana wetu,
Amina.
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
Amina.
Day 4: Patience
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit.
Amen.
Patience
Let us bow down in humility at the power and grandeur of the Holy Spirit. Let us worship the Holy Trinity and give glory today to the Paraclete, our Advocate.
O Holy Spirit, by Your power, Christ was raised from the dead to save us all. By Your grace, miracles are performed in Jesus’ name. By Your love, we are protected from evil. And so, we ask with humility and a beggar’s heart for Your gift of Patience within us.
O Holy Spirit, you give lavishly to those who ask. Please give us the patience of the Saints who are now with you in heaven. Help us to endure everything with an eternal patience that is only possible with your help.
Holy Spirit we ask for the grace of [Mention your intention here].
Amen.
Come Holy Spirit, fill the hearts of your faithful and enkindle in them the fire of your love. Send forth your Spirit and they shall be created. And You shall renew the face of the earth.
O, God, who by the light of the Holy Spirit, did instruct the hearts of the faithful, grant that by the same Holy Spirit we may be truly wise and ever enjoy His consolations, through Christ Our Lord,
Amen.
In the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Spirit.
Amen.