Siku ya 3

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.

Ee Yesu wangu, umesema: “Kweli nawaambia, ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa.”

Tazama ninabisha, ninatafuta, na ninaomba neema ya…

(Taja nia yako hapa)

Moyo Mtakatifu wa Yesu, naweka tumaini langu lote kwako.

Ee Yesu wangu, umesema: “Kweli nawaambia, mkimwomba Baba neno lolote kwa jina langu, atawapa.” Tazama, kwa jina lako, ninamwomba Baba neema ya…

(Taja nia yako hapa)

Moyo Mtakatifu wa Yesu, naweka tumaini langu lote kwako.

Ee Yesu wangu, umesema: “Kweli nawaambia, mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita.” Nikiwa nimetiwa moyo na maneno yako yasiyokosea, sasa ninaomba neema ya…

(Taja nia yako hapa)

Moyo Mtakatifu wa Yesu, naweka tumaini langu lote kwako.

Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambaye haiwezekani usiwe na huruma kwa wanaoteseka, utuhurumie sisi wakosefu maskini na utujalie neema tunayokuomba, kwa njia ya Moyo wenye Huzuni na Usio na Doa wa Maria, Mama yako mpole na Mama yetu.

Amina.

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina.