Litania ya Uso Mtakatifu wa Yesu

Litania ya kuheshimu Uso Mtakatifu wa Yesu, ulioabudiwa kutoka Bethlehemu hadi Msalaba.

Litania ya Uso Mtakatifu wa Yesu

Bwana utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Bwana Yesu, utusikie.
Bwana Yesu, utusikilize.

Kiitikio: Utuhurumie

MUNGU Baba wa mbinguni,
MUNGU Mwana, Mkombozi wetu,
MUNGU Roho Mtakatifu,
MUNGU Mmoja katika Nafsi Tatu,

Kiitikio: Utuhurumie

Uso Mtakatifu wa Yesu ulitwaa Mwili na kuwa Mwanadamu,
Uso Mtakatifu wa Yesu uling'ara Bethlehemu angoni,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioabudiwa na Mama Bikira Maria pangoni,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioabudiwa na Mtakatifu Yosefu pangoni,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioabudiwa na Malaika,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioabudiwa na Wachungaji,
Uso Mtakatifu wa Yesu unaowahurumia wakosefu,
Uso Mtakatifu wa Yesu uliolia machozi ya Damu katika mateso,
Uso Mtakatifu wa Yesu uling'ara na kugeuka mlimani Tabori,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioloweshwa Damu Bustanini Getsemane,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioarijiwa na Malaika katika mahututi yako,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulitemewa mate mara 180,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioarijiwa na Veronika,
Uso Mtakatifu wa Yesu uliodharauliwa sana,
Uso Mtakatifu wa Yesu uliopigwa makofi,
Uso Mtakatifu wa Yesu uliofifia kwa mateso makali sana,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulioumizwa kwa kuchomwa na miiba,
Uso Mtakatifu wa Yesu ambao malaika hupenda kutazama,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulio mwanga wa milele,
Uso Mtakatifu wa Yesu furaha ya Malaika,
Uso Mtakatifu wa Yesu unaotuangazia wote,
Uso Mtakatifu wa Yesu chumba cha kwanza mbinguni,
Uso Mtakatifu wa Yesu unaotutazama kwa wema na huruma,
Uso Mtakatifu wa Yesu jina la milele,
Uso Mtakatifu wa Yesu ulio mpole sana,

Kiitikio: Utuhurumie

Mwanakondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu, Utusamehe Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu, Utusikilize Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu, Utuhurumie.

TUOMBE

Ee Mungu, uliyemtoa Mwanao wa pekee awe Mwokozi wa watu wote, tunakuomba upokee sadaka ya mateso yake makali mno, na usizitazame dhambi zetu bali tu uso mpendevu wa Mwanao wa pekee. Tunaabudu Uso Mtakatifu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Mwokozi wetu, aliye na mapendo yasiyo na mwisho na huruma isiyopimika. Yeye mwenyewe atujalie msamaha wa dhambi zetu, nasi tuufariji uso wake Mtakatifu kwa kuishi vyema na kuishuhudia imani yetu kwa mapendo bila hofu. Amina.

Ee Uso Mtakatifu uliotoka damu, Ee Uso Mtakatifu wa Bwana Yesu, uabudiwe milele. Amina.

litaniauso mtakatifuyesumatesoveronika

← Back to Litanies