Litania ya Roho za Toharani

Litania ya kuombeleza roho za waamini marehemu katika toharani.

LITANIA YA ROHO ZA TOHARANI

Bwana utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Yesu utusikie.
Yesu utusikilize.

Baba wa Mbinguni Mungu,
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu,
Roho Mtakatifu Mungu,
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja,
Wahurumie roho za waamini marehemu.

Maria Mtakatifu,
Mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Mtakatifu Mikaeli,
Mtakatifu Gabrieli,
Enyi Malaika na Malaika Wakuu,
Mt. Yohane Mbatizaji,
Mtakatifu Yosefu,
Enyi Mababu na Manabii,
Mtakatifu Petro,
Mtakatifu Paulo,
Mtakatifu Yohane,
Enyi Mitume na Wainjili,
Mtakatifu Stephano,
Mtakatifu Laurenti,
Enyi Mashaidi Watakatifu,
Mtakatifu gregori,
Mtakatifu Ambrose,
Enyi Maaskofu na Waungama,
Mtakatifu Maria Magdalena,
Mtakatifu Kataina,
Enyi Mabikira Watakatifu na Wajane,
Enyi Watakatifu wote wa Mungu,
Waombee roho za waamini marehemu

Uwarehemie,
Uwaokoe Ee Bwana.
Uwarehemie,
Utusikilize Ee Bwana.
Katika Makovu yote,
Uwaopoe Ee Bwana.
Katika Hasira yako,
Katika ndimi za moto,
Katika eneo hilo la uvuli wa mauti,

Kwa kuchukuliwa mimba bila dhambi ya Asili,
Kwa kuzaliwa kwako,
Kwa jina lako Takatifu,
Kwa wingi wa upole na huruma yako,
Kwa mateso yako machungu,
Kwa Majeraha yako Matakatifu sana,
Kwa Damu yako Azizi,
Kwa kifo chako cha aibu, kwa hicho uliangamiza kifo chetu,

Sisi wakosefu,
Twakuomba utusikie.

Ee uliyemsamehe mwanamke na ukaisikiliza sala ya mwizi mwema.
Ili uweze kuwaachilia marehemu wazazi wetu, jamaa na wafadhili wetu kutoka katika vifungo vya dhambi na adhabu zake,
Ili ufanye siku ije haraka ya kuwatembelea waamini wako waliofungwa katika nafsi ya mateso, na uwafikishe katika jiji la amani ya milele,
Ili kwamba utafupisha muda wao wa malipizi kwa ajili ya dhambi zao na kwa wema uwapokee katika madhabahu takatifu, ambamo kamwe kitu kilicho kichafu hakiwezi kuingia.
Ili kwa njia ya Sala na Sadaka za Kanisa lako, na haa kwa sadaka yenye thamani kuu ya Altare yako Takatufu,
Ili uweze kuwapokea katika tabernakulo ya pumziko na tuzo la matumaini yao pamoja na heri isiyo na mwisho, pamoja na Mwana wa Mungu.

Mwanakondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu, Uwajalie pumziko la milele.
Mwanakondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu, Uwajalie pumziko la milele.
Mwanakondoo wa Mungu, aondoaye dhambi za ulimwengu, Uwajalie pumziko la milele.

Bwana utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Kristo utuhurumie.
Bwana utuhurumie.
Bwana utuhurumie.

Sali: Baba yetu . . .
K/ Usitutie kishawishini,
lakini utuopoe maovuni.
K/ Toka kwenye milango ya Jehanamu,
Uziopoe Roho zao Ee Bwna.
K/Wapumzike kwa amani,
Amina
K/ Ee Bwana usikie sala yangu,
Nakilio changu kikufikie.

Tuombe: Ee Mungu mkombozi wa waamini wote, wajalie msamaha wa dhambi zao zote roho za watumishi wako waliotangulia ili kwa maombezi yetu, waweze kupata msamaha ambao daima wameutamani kwa njia ya bwana wetu. Amina
Ee Mungu utoaye msamaha na mpenda wokovu wa watu tunakuomba rehema kwaniaba ya ndugu zetu, jamaa na wafadhili ambao wameondoka katika maisha haya, ili kwa maombezi ya Bikira Maria na ya watakatifu wote, waweze kupokelewa katika furaha za ufalme wako usio na mwissho. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina
Ee Mungu ambaye daima unayo huruma na unapenda kuokoka, tunakusihi uangalie kwa upendeleo uwaangalie roho za warumishi wako na uwajalie msamaha wa dhambi zao zote, ili wakiachiwa kutoka kwenye vifungo vya maisha haya, waweze kupokelewa katika maisha ya milele. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina

litaniatoharaniroho za marehemumarehemu

← Back to Litanies