Litania ya Roho Mtakatifu

Litania ya kumwomba Roho Mtakatifu atutakase, atupe hekima na neema.

Litania ya Roho Mtakatifu

Bwana, utuhurumie.
Kristu, utuhurumie.
Bwana, utuhurumie.

Kiitikio: Utuhurumie

Baba mwenyezi,
Ahadi ya Mungu Baba,
Mwanga wa nuru ya mbinguni,
Mwanzilishi wa mema yote,
Chemchemi ya maji ya mbinguni,
Moto unaoteketeza,
Upendo wenye ari,
Mpako wa kiroho,
Roho wa upendo na kweli,
Roho wa hekima na akili,
Roho wa shauri na nguvu,
Roho wa elimu na uchaji,
Roho wa kumcha Bwana,
Roho wa neema na sala,
Roho wa amani na upole,
Roho wa kiasi na kutokuwa na hatia,
Roho Mtakatifu, Mfariji,
Roho Mtakatifu, Mtakasaji,
Roho Mtakatifu, unayeliongoza Kanisa,
Kipawa cha Mungu Aliye Juu,
Roho unayeujaza ulimwengu,
Roho wa kufanywa watoto wa Mungu,

Kiitikio: Utuokoe

Yesu, Mwana wa milele wa Baba, Mkombozi wa dunia,

Kiitikio: Ututakase

Roho wa Baba na Mwana, Uzima usio na mipaka wa wote wawili,

Kiitikio: Utusikilize

Utatu Mtakatifu,

Kiitikio: Ingia mioyoni mwetu

Roho Mtakatifu, utokaye kwa Baba na Mwana,
Roho Mtakatifu, uliye sawa na Baba na Mwana,

Roho Mtakatifu, ututie chuki kuu ya dhambi.
Roho Mtakatifu, uje uufanye upya uso wa dunia.
Roho Mtakatifu, umwage nuru yako rohoni mwetu.
Roho Mtakatifu, uchore sheria yako mioyoni mwetu.
Roho Mtakatifu, utuwashe kwa mwali wa upendo wako.
Roho Mtakatifu, utufungulie hazina za neema zako.
Roho Mtakatifu, utufundishe kusali vema.
Roho Mtakatifu, utuangalie kwa uvuvio wako wa mbinguni.
Roho Mtakatifu, utuongoze katika njia ya wokovu.
Roho Mtakatifu, utujalie elimu ile tu iliyo ya lazima.
Roho Mtakatifu, utuvuvie kutenda mema.
Roho Mtakatifu, utujalie stahili za fadhila zote.
Roho Mtakatifu, utufanye tudumu katika haki.
Roho Mtakatifu, uwe tuzo letu la milele.

Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Ututumie Roho wako Mtakatifu.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Uimwage rohoni mwetu zawadi za Roho Mtakatifu.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utujalie Roho wa hekima na uchaji.

K. Njoo, Roho Mtakatifu! Uijaze mioyo ya waamini wako,
W. Na uiwashe ndani yao moto wa upendo wako.

Tuombe.

Ee Baba mwenye huruma, utujalie Roho wako wa kimungu atuangazie, atuwashe na atutakase, apenye ndani yetu kwa umande wake wa mbinguni na atufanye tuzae matunda katika matendo mema, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu, Mwanao, aishiye na kutawala pamoja nawe katika umoja wa Roho huyo huyo, milele na milele. W. Amina.

litaniaroho mtakatifuutakatifuhekima

← Back to Litanies