Litania ya Mtakatifu Ana

Litania ya kuomba maombezi ya Mtakatifu Ana, mama wa Bikira Maria Mtukufu.

Litania ya Mtakatifu Ana

Bwana, utuhurumie.
Kristu, utuhurumie.
Bwana, utuhurumie.
Kristu, utusikie.
Kristu, utusikilize.

Kiitikio: Utuhurumie

Baba wa mbinguni, Mungu,
Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu,
Roho Mtakatifu, Mungu,
Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja,

Kiitikio: Utuombee

Maria Mtakatifu, Malkia wa Malaika na Watakatifu,
Mtakatifu Ana, chombo cha Roho Mtakatifu,
Mtakatifu Ana, mwenzi mwaminifu wa Mtakatifu Yoakimu,
Mtakatifu Ana, kioo cha walio katika ndoa,
Mtakatifu Ana, mfano wa wajane,
Mtakatifu Ana, muujiza wa uvumilivu,
Mtakatifu Ana, mama wa tumaini,
Mtakatifu Ana, mama wa uthabiti,
Mtakatifu Ana, mama wa sala,
Mtakatifu Ana, mama wa baraka,
Mtakatifu Ana, chombo cha utakatifu,
Mtakatifu Ana, mama mwenye huruma,
Mtakatifu Ana, mfariji wa wenye dhiki,
Mtakatifu Ana, msaada wa maskini,
Mtakatifu Ana, mlinzi wa mabikira,
Mtakatifu Ana, msaada wa wanaodhulumiwa,
Mtakatifu Ana, kimbilio la wateja wako,

Kiitikio: Tunakuomba, utusikilize

Sisi wakosefu,
Kwa upendo wako kwa Yesu na Maria,
Kwa fadhila na stahili zako,
Kwa wema na huruma yako,
Kwa huruma na mapendo yako,
Kwa neema ulizopewa na Mungu,
Kwa furaha ulizozipata pamoja na Yesu na Maria,
Kwa heri unayoifurahia milele yote,
Kwa heshima unayopewa na Watakatifu mbinguni,

Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utusamehe, ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utusikilize kwa huruma, ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za dunia,
Utuhurumie.

K. Utuombee, Mtakatifu Ana,
W. Tustahili kuzijaliwa ahadi za Kristu.

Tuombe.

Ee Mungu, uliyependa kumjalia Ana mbarikiwa neema ili astahili kuwa mama yake yeye aliyemzaa Mwanao pekee, utujalie kwa huruma kwamba sisi tunaoheshimu kumbukumbu yake kwa ibada, tusaidiwe pia na maombezi yake yenye nguvu. Kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

litaniamtakatifu anamariamaombezi

← Back to Litanies