Matendo ya Uchungu

Jumanne, Ijumaa

  1. Tendo la kwanza: Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
  2. Tendo la pili: Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
  3. Tendo la tatu: Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
  4. Tendo la nne: Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
  5. Tendo la tano: Yesu anakufa Msalabani.Fadhila: Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
← Back to mysteries of the Rosary