Siku ya 1

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Amina.

Ee Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama wa Kanisa, uwe mama yangu na uniongoze katika maisha ya utakatifu ili siku moja niungane nawe na Mwanao mbinguni milele yote. Uniombee ili niwe mwanafunzi wa unyenyekevu na usafi wako. Ninaomba uziweke mbele ya Mwanao haja zangu.

(Taja nia zako hapa)

Maria uliyechukuliwa mimba bila dhambi, utuombee.

Maria Mtakatifu Sana, utuombee.

Maria Msafi Sana, utuombee.

Maria, Nyota ya Bahari, utuombee.

Maria, Malkia wa Mbingu na Dunia, utuombee.

Maria, Malkia wa Malaika na Watakatifu, utuombee.

Amina.

Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Amina.