Shukrani (Sehemu ya Pili)

Siku 3 za kumshukuru Mungu baada ya siku tisa za novena, kabla ya kuendelea Siku ya Kumi hadi Siku ya Kumi na Mbili.

Sehemu ya PILI

Siku 3 za Kumshukuru Mungu kwa Heshima ya Mt. Rita wa Kashia

Baada ya kusali siku tisa (9) za Novena hii kwa Mtakatifu Rita wa Kashia, unaalikwa kusali siku tatu (3) za kumshukuru Mungu kwa heshima ya Mtakatifu Rita.
Shukrani hii ni kwa ajili ya kujibu maombi ya sala zako ulizosali kwa siku 9. Vilevile kumshukuru Mungu kwa kumaliza novena salama hata kama unadhani hujajibiwa ombi lako. Ni wajibu wetu kumshukuru Mungu kila wakati na kwa kila kitu (1 Tes. 5: 18).

Kila siku baada ya kumaliza sala za sehemu hii ya shukrani, unatakiwa kusali pia *Litania ya Mtakatifu Rita wa Kashia au Zaburi ya 51 ya Kuomba Huruma ya Mungu.* Unaweza kuchagua moja ya sala hizo mbili (Litania ya Mtakatifu Rita au Zaburi ya 51).